Mbuga ya Serengeti

1493440606_Mikunizebras-tanzania

Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na nchi ya Kenya.
Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara.
Kuna idadi kubwa ya wanyamapori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama, kati yao “watano wakubwa” wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati.
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya zamadamu yalipatikana liko ndani ya Serengeti.
Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia katika kaskazini-magharibi mwa Tanzania na inaenea kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. Inaenea kiwango cha mraba kilometa 30,000 2.
Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi duniani,[1] ambao hua ni tukio wa nusu mwaka . Uhamiaji huo ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu ya kusafiri.
Kanda hii ina hifadhi za taifa na hifadhi mchezo kadhaa. Jina Serengeti limechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai hasa, “Serengit” kumaanisha “Kiwara kisichoisha”. [2] [3]

Leave a comment

Blog at WordPress.com.

Up ↑